<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Peleleza Ndani Yangu TZR59</title>
<lyrics>[V1]
 Peleleza ndani yangu,
 Iwe safi nia,
 Kwangu kama kwako Mungu,
 Idhihiri pia.

[V2]
 Peleleza moyo wangu
 Uunifunulie,
 Yaliyomo ndani yangu
 Nami niyajue.

[V3]
 Kwanza washe zako tambi,
 Kumefunga giza;
 Nijue ambavyo dhambi
 Ni la kuchukiza.

[V4]
 Peleleza na mawazo
 Ni mbegu za mambo,
 Asili ya machukizo,
 Maumbuo - umbo.

[V5]
 Zidi kuyapeleleza
 Katikati yangu
 Hata wishe nifundisha
 Udhaifu wangu.

[V6]
 Hapo nikikwinamia
 Mbele zako, Mungu,
 Hakika nitakujua
 U mpenzi wangu.</lyrics>
<hymn_number>59</hymn_number>
</song>